Kutengeneza kadi ya mwaliko
Tumia kihariri cha kadi kuchagua muundo wa Shereko au kupakia wako, weka majina ya wageni na picha, acha nafasi kwa QR, kisha jaribu kabla ya kutuma.
Kila mgeni anapokea nakala yake ya kadi, yenye jina lake na QR yake binafsi ya mapokezi vikijazwa vyenyewe. Unaandaa kadi mara moja tu kwenye kihariri cha kadi.
Fungua kihariri cha kadi
Fungua tukio lako kisha bonyeza kichupo cha Kadi. Kihariri kinafunguka na jina la tukio juu, mwambaa wa zana, kadi katikati na zana zako upande wa kushoto. Kwenye simu, zana ziko kwenye mwambaa wa chini.
Vichupo vya zana ni Muundo, Picha, Maandishi na Vipengele. Ukichagua kitu kwenye kadi, kichupo cha Hariri kinaonekana, na Tabaka zinaorodhesha kila kitu kilicho kwenye kadi.
Chagua muundo au pakia kadi yako
Kwenye kichupo cha Muundo una njia mbili za kuanza:
- Miundo ya Shereko: pitia miundo iliyo tayari. Tumia kisanduku cha kutafuta ("harusi, dhahabu, maua…") na vichujio kupunguza, kisha gusa mmoja kuuona na bonyeza Tumia muundo huu. Ukiutumia, unachukua nafasi ya kadi yako ya sasa, lakini unaweza kurudisha.
- Pakia picha yako: una kadi kutoka kwa mbunifu wako? Ipakie. Shereko inaanza upya na jina la tukio pamoja na QR ya mapokezi juu ya picha yako; ongeza taarifa nyingine unazohitaji kupitia Maandishi.
Ongeza maandishi, majina ya wageni na picha
- Maandishi: bonyeza Ongeza maandishi, kisha andika kwenye kadi au kwenye paneli ya pembeni. Tumia Ongeza taarifa kuweka vitu vinavyobadilika kwa kila mgeni au tukio, kama Jina la mgeni, Aina ya tiketi, Wenye Sherehe, Tarehe, Saa au Mahali.
- Fonti na mtindo: chagua mstari wa maandishi kisha tumia mwambaa ulio juu ya kadi kubadilisha fonti, ukubwa, mtindo na mpangilio. Fonti inafungua mkusanyiko uliopangwa kwa Mwandiko, Serif, Sans serif na Za kuchangamsha.
- Picha: kwenye kichupo cha Picha, bonyeza Ongeza picha au mojawapo ya Picha zako. Buruta pembe kubadilisha ukubwa, kingo kukata, na pete kuzungusha.
- Fremu: kwenye kichupo cha Vipengele, gusa umbo kuongeza fremu ya picha, kisha weka picha ndani yake.
- Ondoa mandharinyuma: chagua picha ya mtu kisha bonyeza Ondoa mandharinyuma kumtoa kwenye mandhari. Ni bure, inafanyika kwenye kifaa chako na picha haitumwi popote. Mara ya kwanza inapakua zana (takriban MB 17).
Tumia Tabaka kuona kila kitu, kubadilisha kipi kiwe mbele, au kufuta. Rudisha na Rejesha ziko katikati ya mwambaa wa juu.
Acha nafasi kwa QR ya mapokezi
Msimbo wa mapokezi kwenye kadi ni wa kipekee kwa kila mgeni; wahudumu wa mlangoni wanauskani wageni wanapoingia. Uchague kuuhamisha na kuweka Ukubwa wa QR. Usiuweke juu ya maandishi au picha zenye vitu vingi ili uskaniwe haraka. Soma Mapokezi.
Hakiki, hifadhi na jaribu
- Hakiki: gusa kitufe cha jicho kubadilisha kati ya nafasi za taarifa na maandishi halisi. Fungua mshale pembeni kisha chagua mgeni uone jina lake linavyotoshea. Ni vizuri kukagua majina marefu.
- Kuhifadhi: kihariri huhifadhi chenyewe. Hali iliyo pembeni ya jina la tukio inaonyesha Inahifadhi… kisha Imehifadhiwa. Ukiona Haikuhifadhiwa, kagua mtandao wako kabla ya kutoka.
- Pakua PNG: inahifadhi picha ya kadi kwenye kifaa chako. Kupakua hakutumi chochote.
- Jaribio: inatuma kadi kwenye WhatsApp yako uone hasa kile wageni watapokea. Namba kwenye kitufe inaonyesha majaribio ya bure yaliyobaki; yakiisha, majaribio yanalipwa kutoka kwenye pochi yako.
Ikiwa imekaa vizuri, bonyeza Tuma kadi juu kulia kuchagua ujumbe wa WhatsApp na kuhakiki gharama. Soma Kutuma mialiko.
Maswali ya mara kwa mara
Naweza kubadilisha kadi baada ya kutuma baadhi ya mialiko?
Ndiyo. Hariri na uhifadhi kama kawaida. Wageni waliokwisha kupokea kadi wanabaki na toleo la zamani; utakaowatumia baadaye watapata jipya.
Kwa nini jina la mgeni linakatika?
Baadhi ya majina ni marefu kuliko mfano. Hakiki kwa jina refu zaidi kwenye orodha yako kisha panua kisanduku cha maandishi au punguza ukubwa wa fonti.
Baadhi ya wageni wanaweza kupata muundo tofauti?
Michango ikiwa imewashwa, unaweza kuweka viwango vinavyotuma muundo maalum wa kadi mgeni anapolipa kiasi fulani au zaidi. Aina ya kadi ya mgeni (mfano VIP) inaweza pia kuandikwa kwenye kadi kwa kutumia taarifa ya Aina ya tiketi. Soma Michango na Kuongeza wageni.
Kutengeneza kadi kuna gharama?
Hapana. Kutengeneza, kuhakiki na kupakua ni bure. Unalipa tu unapotuma. Angalia bei.
Je, makala hii imekusaidia?
Bado unahitaji msaada?Timu yetu inajibu WhatsApp na barua pepe, kwa kawaida ndani ya saa chache mchana.
Tuandikie WhatsApp